Friday, September 26, 2014

DIAMOND MWISHOWE AFUNGUKA

Hatimaye Diamond Platnumz amefunguka
kuhusu tetesi zinazoendelea kuwa ameachana
na Wema Sepetu na kwamba ana mpango wa
kufunga ndoa na Meninah Atick.
Diamond ameiambia MAUMBEA DOT COM  kuwa tetesi hizo
zimekuwa zikimhuzunisha kwa kiasi kikubwa.
“Unajua hizi habari kiukweli zimekuwa
zikinihuzunisha sana,” amesema msanii huyo.
“Unajua mie ni mtu mmoja ambaye sipendi
kuzunguzia mambo ya rumors, siju magazeti
huwa sipendi kuzungumzia kabisa, kwa kuwa
najua kabisa siwezi kubishana na media
kwakuwa media ni kubwa, maana najua
utaongea na huyu na yule siku ya siku
utagombana na watu. Ndio maana huwa nakaa
kimya,” ameongeza Diamond.
Wema
“Kusema ukweli hili suala limekuwa likiniumiza
‘eti sijui kuna vikao vya harusi mie nataka
kumuoa Meninah’ Kusema ukweli sina
mahusiano na Meninah. Kila mtu anajua mie
nina mahisiano Wema. Wema ndo mpenzi
wangu, ila wakati mwingine nakuwa naelewa ile
inakuwa ni trick ya kibiashara. Mtu anajua hata
nikimuandika vipi ‘Diamond sijui kafanya nini
watu hawawezi kumchukia! Kwahiyo wanaamua
kunitengenezea chuki na maadui kwa watu kuwa
nipo na mwanamke wangu halafu namsaliti.”

Meninah : “Unajua kitendo hicho hatamaye kinaniudhi
naona mtu yupo na mpenzi wake halafu
anamsaliti. Najua hicho ni kitendo ambacho kila
mtu hakimpendezi. Kwahiyo wanaamua
kunitengenezea chuki na maadui kupitia njia
hiyo. Labda wana wasanii wao, sasa wanaona
tukiingia kwa njia hii tutaweza kuamharibia
Diamond. Ndioa siku zote nimekuwa kimya tu ila
sina mahusiano na Meninah. Mie nikiwa na mtu
huwa sifichi naweka wazi kabisa. Hata kama leo
nimeachana na Wema nasema tu, why nifiche?
Mie katika mambo yangu huwa simuogopi mtu
kama ningekuwa nataka kuoa basi ninge weka
wazi why nifiche?”

No comments:

Post a Comment